Sio kitu cha kawaida sana kwa watu maarufu duniani ukakutana nae na hata kuzungumza na kumuuliza swali lolote unalojisikia akakujibu, mtanzania Benjamin Fernandes anayesoma chuo kikuu cha Stanford Graduate School of Business cha California Marekani amepata bahati ya kukutana na kocha mwenye heshima kubwa England Sir Alex Ferguson.
Benjamin na wanafunzi wenzake wamepata nafasi ya kukutana na kocha wa zamani wa Man United Sir Alex Ferguson wakiwa chuoni hapo na kumuuliza maswali kadhaa ambayo yote aliwapa majibu na kuonesha ushirikiano mkubwa, kubwa Ferguson walimuuliza ni kitu gani muhimu kwa upande wake?
“Tukamuuliza unafikiri kitu gani katika maisha yako ni muhimu akasema malezi ni kitu muhimu sana kwa kila mtu hata kama huna baba wala mama yule mlezi amekufundisha nini? kwa sababu hiko kitu kina kusaidia na yeye alivyokuwa anatafuta wachezaji alikuwa anaangalia mchezaji ana hekima kiasi gani”
Kama humfahamu Benjamin Fernandes ni mtanzania mwenye umri wa miaka 23 kwa sasa anasomea masters ya biashara katika chuo kikuu cha Stanford Graduate School of Business cha California Marekani lakini anafanya kazi katika taasisi ya Melinda & Bill Gates Foundation inayoendeshwa na tajiri wa duniani Bill Gates.
BONYEZA PLAY KUSIKIA MASWALI YOTE WALIYOMUULIZA FERGUSON
VIDEO: Simba imekubali kipigo cha nne cha VPL vs Kagera April 2 2017