Felisiana Raphaeli mkazi wa Kata ya Kibosho Magharibi Wilaya ya Moshi Vijijini Mkoani Kilimanjaro ametimiza umri wa miaka 124 ambapo imefanyika ibada ya shukrani kwa kutimiza umri huo na kisha baadaye kufanyiwa sherehe ya kuzaliwa ‘birthday’ nyumbani kwake.
Mtoto wa mwisho wa Bibi huyo Steven Raphael amesema mama yake alizaliwa amebarikiwa kuwa na watoto nane, wajukuu 22, pamoja na vitukuu 42 lakini hawezi kuzungumza kwa sasa japo ana uwezo wakutembea kidogo pale anapopatiwa msaada.
“Bibi amefikisha umri huo kutokana na matunzo, Babu mzaa bibi alifariki akiwa na miaka 128 uzao wa Bibi unaonekana MUNGU ameubariki” Steve