Mtangazaji wa Televisheni na redio nchini Afrika Kusini mweusi amesema kuwa amekuwa muathiriwa wa shambulio lililochochewa na ubaguzi wa rangi baada ya kusimamisha gari lake kwa ajili ya kulisaidia kundi la wazungu ambao gari lao lilikuwa limepinduka.
Kwa mujibu wa BBC, Samora Mangesi alituma picha zake za majeraha aliyoyapata katika kile alichodai ni shambulio , analosema lilifanyika Ijumaa. Yeye na marafiki zake wawili wa kike waliitwa “nyani”, alisema. Walipoulizwa ni kwanini wanatukanwa, walipigwa hadi wakapoteza fahamu.
Wakati wa tukio hilo lililotokea Mjini, Mangesi, ambaye ni mtangazaji wa shirika la habari la Afrika Kusini ABC, amesema alipata majeraha usoni mwake na mwili wake ulikuwa na damu baada ya kupigwa mateke alipokuwa amelala chini.
“Hata wakati nilipokuwa nikiwekwa kwenye gari la wagonjwa, mmoja wa jamaa hawa alijaribu kupita juu ya mwili wa mmoja wa rafiki zangu na gari yake aina ya pick-up ikabidi madaktari waingilie kati .” Mangesi.
“Licha ya kwamba walisema nilizinduka, sina kumbukumbu nikiwa ndani ya gari la wagonjwa, nilivyofika hospitalini na hata sikumbuki mengi kuhusu matibabu yangu .”
Alifikiria juu ya “kusahau yaliyompata na kuendelea na maisha yake”, lakini sasa ameripoti tukio hilo kwa polisi” aliongeza Mangesi