Rais wa zamani wa FIFA Sepp Blatter leo December 5 2016 ameingia tena kwenye headlines, hiyo ni baada ya rufaa yake aliyoikata katika mahakama ya kimichezo CAS kupinga kutumiakia adhabu ya kifungo cha miaka 6 kutojihusisha na soka kukataliwa.
Blatter alifungiwa miaka sita kujihusisha na soka kwa makosa mbalimbali ya kimaadili ikiwemo kufanya malipo yasio ya kihalali ya pound milioni 1.3 kwa Rais wa zamani wa UEFA Michel Platini, kiasi ambacho kinadaiwa kilitumika kumpigia kampeni Blatter.
Baada ya rufaa yake kukataliwa Blatter aliongea hivi “Nalazimika kukubaliana na haya maamuzi nimekuwa nikifanya kazi FIFA kwa miaka 41, kikubwa nilichojifunza katika michezo ni kuwa unaweza kushinda na unaweza kushindwa”
ALL GOALS: Simba vs Toto Africans October 23 2016, Full Time 3-0