Baada ya Mwimbaji Ben Pol kuachia wimbo wake mpya aliomshirikisha Darassa, wimbo ambao alianza ku-promote ujio wake kwa kupost picha akiwa bila nguo, kumekua na mapokezi ya tofautitofauti kutoka kwa watu mbalimbali kutokana na picha hizo alizozitanguliza.
Baada ya kuusikia wimbo huo, Mwimbaji Baraka The Prince ametumia ukurasa wake wa Instagram kuandika masikitiko yake >>>Nimekuwa disappointed sana huu wimbo… kwa jamaaa alivyojitoa nilidhani ni kitu kikubwa kumbe upumbavu’ #saveourmusic
Wewe pia unaweza kuusikiliza na kupakua wimbo huo mpya wa Ben Pol kupitia kwenye Link iliyopo kwenye Bio yake ya Instagram na kuniandikia maoni yako hapa mtu wangu lakini kama ulipitwa na alichosema Ben Pol kuhusu hizo picha, bonyeza play hapa chini kutazama video nzima.