Baada ya Mitambo ya Clouds kuwashwa na kurudi hewani tena baada ya siku 7 za adhabu ya TCRA, Mkuu wa Maudhui Clouds Media Sebastian Maganga ameelezea uboreshaji wa vipindi walioufanya na jinsi Shangazi Biggie alivyowatuma kuwatumia Mashabiki.
Seba amesema kwenye hizo siku 7 za ukimya hawakwenda likizo bali walijifua zaidi na kujipanga kurejea upya, kuhusu ujio wa kipindi mbadala wa Jahazi amesema ni kweli Wasikilizaji watarajie hilo kuna ujio wa kipindi kipya na itategemea Watangazaji wanaweza kuwepo walewale au wakaongezeka.