BreakingNews

BREAKING: Freeman Mbowe arudishwa Polisi usiku huu

on

Sakata la dawa za kulevya bado lipo kwenye vichwa vya habari Tanzania ambapo Jumatatu ya February 20 2017 imemuhusu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Freeman Mbowe aliyefika Polisi kwa mahojiano.

Jioni ya Jumatatu Mbunge huyo wa Hai Kilimanjaro alichukuliwa na Polisi kwenye msafara wa magari yasiyopungua matatu ambapo iliripotiwa baadae kwamba Polisi walikwenda kufanya upekuzi kwenye nyumba zake Kawe na Mikocheni kwa mujibu wa Afisa habari wa CHADEMA.

Msemaji huyo wa CHADEMA Tumaini Makene alithibitisha Polisi kupekua nyumba zake na kuandikisha maelezo ya majirani ambapo akasema kwenye mida ya saa sita usiku huu Polisi wamemrudisha Mbowe kwenye kituo cha Polisi kati na wamemfungulia jalada la Uchunguzi….. tunaendelea kufatilia zaidi

Endelea kukaa karibu na millardayo.com na AyoTV utaendelea kupata taarifa za kila kinachoendelea kwenye anga la Tanzania na nje ya Tanzania, hakikisha ume-Install APP ya “millardayo” pia kufollow Facebook, Twitter, Instagram na Snapchat kwa jina hilohilo la @millardayo ili upate kila BREAKING NEWS.

Mbowe amerudishwa Polisi Kati DSM usiku huu baada ya kupekua nyumba zake Mikocheni na Kawe, msemaji wa chama athibitisha. #MillardAyoUPDATES

Unapotangaza Mtu aje Polisi saa 5, wewe ni nani? – MBOWE….. Bonyeza play hapa chini kutazama

VIDEO: Rais Magufuli tena kuhusu sakata la dawa za kulevta, agizo jipya la Rais Magufuli kwa Watanzania waliofungwa nje kwa dawa za kulevya, bonyeza play hapa chini

BREAKING NEWS zote na stori za mastaa utazipata kwa Reporter wako MillardAyo, hakikisha umejiunga na mimi kwenye Facebook, Twitter, Instagram, Snapchat, Youtube, APP kwenye ANDROID na IOS kote huko kwa jina hilohilo la @millardayo

Soma na hizi

Tupia Comments