Michezo

BREAKING: Barcelona watangaza kuachana na Messi

on

Club ya FC Barcelona imetangaza kuwa staa wao raia wa Argentina Lionel Messi hatoendelea tena kuitumikia FC Barcelona licha ya club na mchezaji kufikia makubaliano ya kubaki.

Barcelona wametangaza kuwa wanalazimika kumuachia Messi aondoke kwa sababu sheria za matumizi ya kifedha kwa vilabu vya LaLiga ndio imeleta kikwazo.

Messi (34) ameitumikia FC Barcelona karibia kipindi chote cha maisha yake, Messi alianza kuichezea timu za vijana za Barcelona toka 2003 alipojiunga nayo akitokea Newell’s Old Boys ya kwao Argentina na mwaka 2004 ndio akaanza kucheza timu ya wakubwa ya Barcelona.

Soma na hizi

Tupia Comments