AyoTV

VIDEO: Majibu ya Waziri mkuu bungeni kuhusu mikataba serikali ya Tanzania inayoingia

on

Mkutano wa tatu, kikao cha sita umeendelea tena leo April 28 2016 bungeni Dodoma, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kayajibu baadhi ya maswali kutoka kwa Wabunge, moja ya swali kutoka kwa Mbunge wa viti maalum CHADEMA  Kunti Yusuph Majala.

Bunge ndio chombo pekee kinachoweza kuishauri na kuisimamia serikali lakini serikali imekuwa ikiingia mikataba ya uwezekezaji bila bunge kushirikishwa, ni chombo gani kimewekwa kuisimamia serikali?

Majibu ya Waziri Mkuu Majaliwa >>>Ni kweli Bunge linafanya kazi ya kuisimamia serikali lakini yapo maeneo ambayo Bunge lenyewe limetoa mamlaka kwa serikali kuendesha shughuli zake kwa kufata taratibu’

‘Utaratibu ambao umewekwa kikatiba, tumemtumia mwanasheria mkuu wa serikali kupitia mikataba yote kuhakikisha haina dosari kisha airuhusu maana bunge lingekua linaletewa mikataba yote basi bunge litakua linafanya kazi ya kupitisha mikataba tu‘ – Waziri mkuu Majaliwa

Kwa muendelezo zaidi unaweza kutazama hii video hapa chini….

ILIPITA HII YA ZITTO KABWE KUHUSU BAJETI IJAYO YA SERIKALI TZ ‘HATUKUTEGEMEA HIVYO AWAMU YA TANO?

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments