Staa wa muziki kutokea Nigeria Davido ambaye pia ni mmiliki wa record label ya Davido Music World Wide (DMW) ametangaza kuachia Album yake ya nne September 2018.
Davido album yake ya kwanza aliachia 2012 Omo Baba Olowo, The baddest 2015 ya tatu Son of Mercy- EP 2016, Davido amelithibitisha hilo alipokuwa akipokea tuzo yake ya msanii bora wa mwaka 2018 katika tuzo za Headies zilizofanyika usiku wa Jumamosi May 5 2018 Lagos Nigeria.
Usiku wa tuzo hizo Davido alibahatika kushinda tuzo tatu za Msanii bora wa mwaka, Wimbo bora wa Pop na wimbo bora wa Mwaka, kama utakuwa unakumbuka vizuri Vanessa Mdee aliteuliwa kuwania tuzo za Headies katika kipengele cha msanii bora ambaye sio Mnigeria na anaushawishi katika soko la muziki nchini Nigeria.
Kwa upande wa kipengele hicho alichokuwa anawania Vanessa Mdee ameshinda msanii Nasty C kutokea South Africa ambapo alikuwa akishindanishwa na wasanii kama Sarkodie(Ghana), Casper Nyovest(South Africa) na Sauti Sol (Kenya)
Steve Nyerere “Maisha yamekuwa Magumu lini kwako yamekuwa mepesi”