Benki yako NMB imezindua rasmi tawi la Buzuruga mkoani Mwanza tawi hili likiwa ni tawi la tisa kuzinduliwa katika mkoa wa huo huku NMB ikiendelea kuwa ndo benki yenye matawi mengi zaidi Tanzania.
Akizungumza katika sherehe ya ufunguzi huo Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mh. Baraka Konisaga ameipongeza benki ya NMB kwa hatua nyingine iliyopiga kwa kusogeza zaidi huduma kwa wateja na kuitaka iendelee kuwa kinara wa huduma za kibenki nchini.
Aliwahamasisha wafanyabiashara,wakulima na wafanyakazi waitumie fursa ya kuwepo kwa tawi la NMB Buzuruga kukidhi mahitaji yao ya kibenki vilevile amewasihi wananchi waache kuweka fedha kwenye chaga za vitanda na badala yake watumie njia salama ya kuweka fedha benki.
Kwa upande wake Bw.Straton Chilongola ambae ni Meneja wa NMB Kanda ya Ziwa amesema>> “Tangu kuanzishwa kwa tawi hili tumeshuhudia wakazi wengi wakija kufungua akaunti na kutumia huduma za benki hii,hii ni uthibitisho kuwa wakazi hawa walikua na kiu ya kupata huduma za kibenki karibu kariba na milangoni kwao Lakini pia tutaendelea kubuni mbinu mbalimbali zitakozotuwezesha kuwafikia wateja wetu karibu zaidi ili kuondoa msongamano kwenye matawi na pia kuokoa muda wa wateja ili waweze kutumia muda wao kwa shughuli endelevu.”
Tawi hili la Buzuruga linatoa huduma zote za kibenki ikiwa ni pamoja na huduma ya mikopo ya aina mbalimbali bila kusahau mikopo ya Kilimo,tawi hili litakua wazi kila Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa mbili na nusu asubuhi hadi saa kumi najioni ( 2:30 asubuhi – 10:00jioni) na Jumamosi kuanzia saa mbili na nusu asubuhi hadi saa sita na nusu mchana (2:30 asubuhi – 6:30 mchana) Jumapili na siku za Sikukuu hakutakuwana huduma ndani ya tawi hili.