Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) limetupilia mbali rufaa ya Tunisia juu ya mchezo wao dhidi ya Mali kwenye michuano ya Afcon kundi F kumalizwa mapema kabla ya dakika 90 kuisha ,mchezo uliochezeshwa na mwamuzi Mzambia Janny Sikazwe na kumalizika kwa Mali kuibuka na ushindi wa 1-0.
Upande wa FTF , Mapema siku ya Alhamisi kupitia tovuti ya chama cha soka nchini Tunisia (FTF) walitoa taarifa kupitia kwa Hussein Jenaieh ikisisitiza “Tutafanya chochote ili kulinda haki ya timu yetu ya taifa ,sisi sio watoto wadogo”.
Afisa mwamuzi wa CAF Essam Abdul Fattah aliviambia vyombo vya habari vya Misri kwamba mwamuzi alipigwa na jua hali iliyoathiri maamuzi yake katika mchezo huo “Baada ya mchezo, alihitaji kwenda hospitali kwa sababu hali ya hewa ilikuwa ya joto sana” amesema Fattah