Headlines za uchaguzi mkuu 2015 bado zinazidi kuchukua nafasi, tumekuwa tukiona watu maarufu kama wasanii wa filamu na Bongofleva wakionyesha hisia zao kwa wagombea wawapendao. Ila kwa wachezaji mpira wa miguu ni tofauti kidogo kulingana na sheria za vilabu vyao pamoja na mikataba yao.
Baada ya kuonekana kwa picha ya nahodha wa klabu ya Yanga na timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars Nadir Haroub Cannavaro akimsuport moja kati ya wagombea Urais wa mwaka 2015, kumekuwa na stori nyingi sana kuhusiana na sheria ya wachezaji kuonesha hisia zao kwa vyama wavipendavyo hususani wakiwa wamevaa jezi za vilabu vyao.
Ripota wa millardayo.com alipata nafasi ya kufanya exclusive interview na katibu mkuu wa Yanga Dk Jonas Tiboroha na kuzungumzia kuhusiana na Cannavaro kuvaa jezi za Yanga na kupiga picha akionyesha hisia zake kwa mgombea huyo.
“Mimi nafikiri Cannavaro angekwenda akiwa amevaa nguo zake za kawaida na kuonyesha kumsuport Magufuli au mwingine isingekuwa na tatizo. Sisi tunachozungumzia ni yeye kuvaa jezi ya klabu na yenye nembo ya mdhamini wetu halafu unaonyesha kushabikia siasa, Cannavaro amekosea hivyo kama klabu tumekaa chini na tutaangalia hatua za kinidhamu zipi zichukuliwe”>>> Cannavaro
Hii ni sauti ya Dk Jonas Tiboroha
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos