Mix

VIDEO: ‘Msiwaogope wanajeshi, wapeni ushirikiano’ – Mkuu wa Majeshi Tanzania

on

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Jenerali Venance Mabeyo amewaondoa hofu wananchi wanapokutana na wanajeshi wanatakiwa kuwa na amani kwasababu wanatokana na watanzania hivyo wawachukulie kama ndugu zao na hawana nia mbaya yoyote

CDF Mabeyo ameyasema hayo akiwa ziarani mkoani Kagera kukagua maendeleo ya kurejesha miundombinu inayotengenezwa na vikosi vya jeshi baada ya  tetemeko la ardhi lililotokea mkoani humo September 10, 2016.

Mkuu wa Majeshi ametembelea kata ya Ishozi wilaya ya misenyi panapojengwa kituo cha afya na shule ya sekondari Omumwani panapojengwa mabweni.

VIDEO: Ilikupita hii ya Makomando wa Tanzania walivyoonesha uwezo mbele ya Rais Magufuli? Bonyeza play kutazama hapa

Soma na hizi

Tupia Comments