Ni story ya namna yake, pata picha mtoto wa miaka minne anapiga simu namba ya dharura 911 hospitali kuomba huduma ya ambulance kwa kuwa mama yake alikuwa ameshikwa uchungu anakaribia kujifungua!
Mtoto huyo Calise Manning wa Michigan, Marekani alijieleza hivi; “mama anatikisika na ana mtoto… Mama yangu ni mjamzito na ana mtoto.. anahitaji msaada…”
Mama wa mtoto huyo Centerria Manning alikuwa na ujauzito wa miezi tisa, alianguka kutokana na kifafa na kilichomuokoa ilikuwa ni namna alivyomfundisha mtoto wake kuomba msaada wakati ikitokea hali kama hiyo.
Mtu aliyepokea simu hiyo alikuwa na shaka juu ya umri wa anayeongea naye, akauliza umri wa Calise, akajibu “Nina miaka minne… nakaribia kuwa mkubwa”
Mama yake anajivunia Celise, anasema amekuwa akimfundisha jinsi ya kuomba msaada inapotokea dharura yoyote tangu akiwa na miaka miwili.
Mtoto huyo alihojiwa akiwa hospitali, anasema alichojisikia furaha zaidi ni kuwa ndani ya ambulance na mama yake ambaye alijifungua mtoto wa kiume, akampa jina T.J.
Siku ya Jumapili mtoto huyo alipewa tuzo maalum kanisani kwa kitendo chake cha kishujaa.
Nimeshea na wewe video yaa story hiyo mtu wangu. Mcheki Celisa hapa!
https://www.youtube.com/watch?v=p17kaPAK2ZE
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter , Instagram, na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza>>> twitter Insta Facebook