Michezo

Cesc Fabregas aomboleza shambulio la Paris kwa namna tofauti, cheki video ya alichokifanya …

on

Tukio la kigaidi lilitokea Ijumaa ya November 13 Paris Ufaransa bado litakuwa gumu kufutika vichwani kwa watu hasa ukiangalia idadi ya watu 129 walipoteza maisha na majeruhi kutajwa kuwa wengi zaidi, ila November 16 kiungo wa kimataifa wa Hispania anayekipiga katika klabu ya Chelsea ya Uingereza Cesc Fabregas kaomboleza kwa stahili yake.

cesc_fabregas_2631783b1

Fabregas ambaye alikuwa mchezaji bora wa mchezo kati ya Hispania dhidi ya Uingereza na timu yake ya Hispania kufanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 2-0, ushindi ambao alishindwa kufurahia baada ya mechi kutokana na tukio la Paris kugusa watu wengi zaidi, Fabregas aliamua kuomboleza Madrid Hispania nje ya Ulabalozi wa Ufaransa kwa kuchukua mpira wa mechi aliyousaini, mishumaa na maua na kwenda kuweka nje ya Ubalozi wa Ufaransa katika jiji la Madrid.

Fabregas-Chelsea-547156

Tukio la Fabregas ambaye amewahi kuchezea vilabu vya Arsenal na FC Barcelona kabla ya mwaka 2014 kuamua kujiunga na Chelsea ya Uingereza, aliamua kufanya hivyo kama sehemu ya maombolezo ya tukio la Paris. Tukio la shambulizi la kujitoa muhanga lilitokea nje ya uwanja wa Stade de France wakati wa mchezo kati ya Ufaransa na Ujerumani.

Sekunde 27 za video ya maombolezo ya Fabregas

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye TwitterFB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE.

Tupia Comments