Taarifa za wiki iliyopita zilieleza kuwa takriban wachimbaji 50 walifukiwa na kifusi baada ya mgodi mmoja wa dhahabu kuporomoka katika Mji wa Kamituga.
Meya wa Kamituga, Alexandre Bundya amesema kuwa hadi sasa haifahamiki ni Wachimbaji wangapi walikuwa wakifanya shughuli zao kwenye mgodi huo.
Mgodi huo uloanguka ulikuwa ukiendeshwa na Kampuni ya Kamituga Mining ambayo ilipewa kazi na Kampuni ya Banro ya Nchini Canada.
Hata hivyo Kampuni ya BANRO alisitisha shughuli zake mwaka jana na kuwaachia wachimbaji wadogo wadogo.