Michezo

Kuna ukweli wowote eti Kombe la FA limebadilishwa jina??

on

cup-fa-trophy_3256663

Michuano ya Kombe la FA ina ukongwe wake wa kutosha kabisa kwenye Historia ya Soka la Dunia.. mpaka sasa imetimiza jumla miaka yake 144 tangu kuanzishwa kwake.

Habari mpya kutoka ndani ya bodi ya kombe la hilo la FA ni kwamba kwa sasa kuna mabadiliko kwenye jina kutoka FA Cup na kwa sasa litakuwa linaitwa Emirates FA Cup kufuatia mkataba mnono wa paundi milioni 30 ambao FA wameingia na Kampuni ya Emirates kwenye udhamini wa ligi hiyo.

Bodi ya FA imeingia mkataba  na kampuni ya Emirates Airlines kwa miaka mitatu, kesho itatangazwa rasmi juu ya mabadiliko rasmi.

Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa>>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Tupia Comments