May 23 2014 mwanamuziki kutoka kundi la muziki wa dance Tanzania Mapacha Watatu Khaleed Chokoraa ambae ni mshindi wa tuzo za KTMA pia, alitangaza rasmi kwenye AMPLIFAYA ya CLOUDS FM kwamba pamoja na kufanya muziki, sasa ni ramsi kwamba kazi yake nyingine mpya itakua ni ngumi za kulipwa ulingoni.
Kwa karibu miaka 7 anasema amekua akifanya mazoezi kujiweka sawa kimwili na kujiandaa kuwa bondia manake alikua anaona ndoto hii lazima itimie.
Kweli imetimia May 24 2014 ambapo alipambana na bondia kutoka Tanga (96.0 CloudsFM) Abdul Manyenza ambae alipigwa na Chokora kwenye round ya kwanza tu na hivyo msanii huyu kuvunja rekodi aliyoitangaza AMPLIFAYANI kabla kwamba anataka kupiga mtu kwenye round za kwanzakwanza tu.
AyoTV ambayo sasa inapatikana kwenye twitter kwa jina la @AyoTV inakuletea dakika 4 za pambano lenyewe lilivyokua mpaka Khaleed akatangazwa mshindi kwenye ukumbi wa friends corner Manzese Dar es salaam.
Unapenda stori kama hizi zisikupite? niko tayari kukutumia wakati wowote mtu wangu, jiunge na mimi kwa kubonyeza >>> Twitter Instagram facebook na kupata pichaz, video, stori na mengine yote ya hii dunia.