Marekani na China ni miongoni mwa nchini ambazo kwasasa ziko katika mgogoro baada ya kuingia kwa ugonjwa Corona Virus, Sasa leo Mei 20, 2020 kupitia msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje aitwae Hua Chunying amezungumza.
‘USA ilisema ina mgonjwa mmoja wa corona wakati Wuhan inaanza lockdown January 23, USA ikawa na maambukizi 1896 wakati China inatangaza dharura ya kitaifa March 13, sasa hivi USA ina vifo zaidi ya Elfu 93, nani kati yetu anapaswa kuwajibika”-Hua Chunying, Msemaji Wizara ya Mambo ya Nje China
‘Uzushi ambao Marekani inausambaza kutushambulia China,utawapotosha Watu kwa muda tu ila mwisho wa siku ukweli utajulikana, Wanasayansi Marekani wameanza kutafuta chanjo ya corona Jan 11 mwaka huu ila kulikuwa na ripoti za maambukizi tangu November mwaka jana, walikuwa wapi?”-HUA
‘Marekani wanatumia mtindo wa sayansi na Demokrasia inayosema ‘fuata nitakacho utaishi, nipinge ufe’, lakini historia inathibitisha kwamba ukijifunza kusoma alama za nyakati na ukazifuata utafanikiwa kupiga hatua, zama zimebadilika, China haiwezi kufa kisa kupingana na USA’-HUA