Habari za Mastaa

Siku Rihanna na Karrueche Tran walikutana uso kwa uso ilikuaje? Chris Brown mwenyewe anaongea (+audio)

on

Kuna kipindi Chris Brown aliweka headlines za kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na wanaweke wawili, Rihanna na Karrueche Tran kwa wakati mmoja, na mwishoni wa mwaka 2012 msanii huyo alionekena pande za Australia na Karrueche akispend Christmas na siku ya Valentine tarehe 14 February ya mwaka 2013 Chris alionekana Marekani na staa wa muziki wa R&B Pop Rihanna!

meetup

Chris Brown.

Nimekutana na interview moja ambayo Chris Brown alishawahi kufanya na humo ndani staa huyo alizungumza kitu ambacho sikuwahi kukijua… Chris alifunguka kuhusu kuwa kwenye mahusiano na wanawake wawili aliowapenda sana, ila kikubwa zaidi alichokigusia Chris ni issue ya Karrueche Tran na Rihanna kukutana uso kwa uso kwa mara ya kwanza kwenye moja ya party aliyokuepo… ilikuaje?! Chris Brown aliisogeza stori kama hivi..

meetup3

Rihanna & Karrueche Tran.

>>> “Kuna kipindi nilienda nje ya nchi nadhani ilikuwa ni Cannes, na ilikuwa ni kipindi ambacho nilikuwa na mpenzi lakini bado ninaongea na kuwasiliana na Rihanna… so nilienda huko kwa ajili ya kushoot video, badaae wakarusha bonge la party kwenye boti na girlfriend wangu alikuwepo, na kama dakika 15 badaae Rihanna akaja nikasema mungu wangu hapa nitafanyaje!!… Lakini unajua nini walikuwa poa wenyewe, wakasalimiana vizuri japo nilikuwa naombaa sana wasiparuane, nilikuwa naomba sana… ila walikuwa wastaarabu sana na hiyo ndio siku ambayo nilijua wananipenda…” <<< Chris Brown.

Nimeisogeza pia sauti ya Chris Brown akielezea mwenyewe jinsi picha nzima ilivyokuwa hapa chini. Bonyeza play kusikiliza.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments