Club ya Simba SC ambao ndio Mabingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania bara msimu wa 2018/2019, leo August 2 2019 wamepokea zawadi yao ya Ubingwa kutoka kwa wadhamini wao SportPesa, Simba SC wamepewa zawadi ya Tsh Milioni 100.

Zawadi ya Simba SC ipo kimkataba kati yao na wadhamini wao wakuu SportPesa kuwa watakuwa wanapokea kiasi fulani cha pesa endapo watakuwa wanafanikiwa kufikia mafanikio flani hususani kutwaa mataji mbalimbali.

VIDEO: Kauli ya Kaseja baada ya kuichezea Taifa Stars baada ya miaka 6