Habari za Mastaa

Unadhani kufanya COLLABO na staa DAVIDO ni kama shilingi ngapi hivi? Hapa kaongelea hilo..

on

Davido-DiamondFans wa muziki ni mashuhuda wa Collabo kali ambazo staa wa Nigeria, DAVIDO ameshiriki na kuzifanya kuwa nyimbo kubwa Afrika na Duniani, sikuwahi kusikia juu ya kiwango cha pesa ambacho analipwa ili kufanya collabo, unaweza kuhisi anahitaji pesa kiasi gani ili afanye collabo yoyote?

Kwenye moja ya interview alizofanyiwa hivi karibuni Davido amesema anafanya muziki kwa sababu anaupenda, haitaji malipo yoyote kutoka kwa msanii ambaye anafanya naye Collabo, hakumbuki kama aliwahi kuhitaji malipo kwa ajili ya kushirikishwa kwenye ngoma yoyote.

I don’t charge for collabos, and I don’t think I have in the past. The truth is I love music and I just do it out of the love. So, I do it for free”– Davido.

Mbongo Fleva wetu DIAMOND PLATNUMZ ni mmoja ya mastaa ambao walipata nafasi kufanya collabo na DAVIDO na ikawa hit kubwa Afrika 2014.

Enjoy kwa kucheki hizi baadhi ya zile Collabo ambazo Davido yumo na zimefanya poa …

Diamond ft. DavidoNumber One Rmx

Runtown ft. DavidoGallardo

Kesh ft. DavidoShoki Rmx

Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook

Tupia Comments