Barabara kuu inayounganisha Mikoa ya Mbeya na Tabora ambayo ilifungwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila kwa muda wa wiki mbili kutokana na Daraja la Mto Lupa kuvunjika na kusababisha baadhi ya wananchi kupoteza maisha, imefunguliwa baada ya ukarabati wa daraja hilo kukamilika.
Barabara hiyo imefunguliwa na DC Chunya, Mhandisi Maryprisca Mahundi kwa niaba ya Chalamila baada ya Wakala wa Barabara nchini (Tanroads) Mkoa wa Mbeya kukamilisha ukarabati wa Daraja hilo ambapo Mkuu huyo wa Wilaya ameagiza magari yenye uzito wa zaidi ya tani 10 yasipite kwenye daraja hilo.