Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars tayari imewasili Khartoum Sudan kwa ajili ya mchezo wake wa marudiano wa kuwania kufuzu kucheza fainali za CHAN 2020 dhidi ya Sudan, Taifa Stars itacheza mchezo huo October 18 2019 ikiwa inahitaji kupindua matokeo.
Baada ya mchezo wao wa kwanza jijini Dar es Salaam kupoteza 1-0, hivyo Tanzania kama inahitaji kusonga mbele itahitaji ushindi wa walau magoli mawili kwenda juu, kuelekea mchezo huo nahodha namba tatu Erasto Nyoni amethibitisha kuwa wamewasili salama na hakuna mchezaji yoyote ambaye ana majeruhi yeye pamoja na wachezaji wenzake wanaomba sapoti ya dua kutoka kwa watanzania.
VIDEO: Bondia wa kambi ya Manny Pacquiao kumfuata Mwakinyo TZ Nov 29