Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, DC Paul Makonda leo September 30 2015 kakatisha kwenye baadhi ya maeneo ndani ya Wilaya ya Kinondoni eneo la Mikocheni ambako kuna Garage za Magari pamoja na Viwanda vidogovidogo.
Garage na Viwandani ni moja ya maeneo ambayo huwa kunakuwa na mazingira ambayo yanakuwa na uchafu mwingi sana kutokana na aina ya shughuli zinazofanyika huko, ishu ya Kipindupindu je?
Idadi ya Wagonjwa waliolazwa Hospitali wakiugua ugonjwa huo inatajwa kuongezeka, hiyo ni moja ya sababu iliyofanya DC Paul Makonda kupita maeneo hayo na kutoa tahadhari.
Kingine ni ishu ya Mikataba kwa wafanyakazi wa Garage na Viwanda vidogo… Hizi ni sentensi zake kuhusu hayo mawili ikiwemo agizo la kujengwa Kantini za Wafanyakazi >>> “Huwezi kuwafanya watu wote hawa wakale mtoni… Ikifika Ijumaa hawa vijana wawe na Mikataba, nitakuja mimi mwenyewe kuwakabidhi.. haiwezekani wawe vibarua wa kudumu”
Hapa alitoa tahadhari pia za kuchukua kuhusu ishu ya Kipindupindu >>> “Jitahidi hata kama uko kwenye mazingira magumu hakikisha unalinda afya yako, iko njia hata kwenye mazingira magumu kutunza afya yako”
Maagizo ya DC Paul Makonda yako kwenye hii sauti pia mtu wangu.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenyeTwitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE