Tukiwa bado katika headlines za Uchaguzi 2015 kumekuwa na matukio mbalimbali yanayotokea kama kuondolewa kwa mabango au kuhusiana na wagombea kuzidisha muda katika kampeni zao sasa leo Sept 30, 2015 mwenyekiti wa tume ya Uchaguzi ameyajibu mbele ya waandishi wa habari.
‘Lakini kwa hili tunajaribu kurudia kurudia kwa hapa ningependa kuchukua nafasi hii walianza kampeni pale Jangwani ambao ni CCM walizidi muda na ikafuata sehemu nyingine pale Morogoro kukawa na malalamiko tulikemea kabisa kwamba lazima wazingatie muda uliotajwa katika muongozo huo’ – Damian Lubuva
‘Kuna kipindi ambazo chama Fulani kimekuja na kulalamika kwamba mbona wenzetu wamefanya kampeni kanisa mara wanaondoa mapango yetu sasa tuliona kwamba katika hali kama hiyo tulichokifanya tumewaita CCM na Chadema wamekuja ofisini mimi na makamishna tukakaa nao tukawaambia walichokifanya hiki sio kizuri na wao walikiri basi tukasema kwamba wakiendelea tutachukua hatua za kisheria’ – Damian Lubuva
‘Kwa hiyo nataka kuiweka wazi kwamba sisi hatukufunga macho kwa chama chochote wale ambao wanaleta tunapeleka katika kamati ya maadili, tunakubaliana kwamba ni suala ambalo utashi wawote wanahusika unatakiwa vyama 22 wametia saini kukubali kwamba wanapoenda kwenye kampeni kuna vitu vinavyotakiwa kuzingatiwa, kwa mfano suala la kuondolewa kwa mapango kuna maeneo mengine ya chama Fulani unakutana mapango yanaondolewa hao wote tumewakemea‘ – Damian Lubuva
Unaweza ukabonyeza play kumsikiliza Mwenyekiti wa tume ya Uchaguzi, Jaji Damian Lubuva
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE