Kundi la Destiny’s Child liliundwa na Beyonce Knowles, Kelly Rowland pamoja Michelle Williams na kuamua kusambaratika huku kila mmoja akijitegemea na kuendelea na kazi zake za muziki.
Mara ya mwisho kundi hili walishirikiana mwaka 2013 lakini unaambiwa mwishoni mwa wiki iliyopita waliungana tena katika tuzo za 30 za kila mwaka za muziki wa injili za Stellar zilizofanyika katika ukumbi wa Orleans Arena, Las Vegas.
Wadada wo walipanda jukwaani na kuimba pamoja wimbo wa “Say Yes” ambao ni wa Michelle aliowashirikisha wenzake.
Wimbo huo ulishinda vipengele vitatu ikiwemo wimbo bora wa mwaka na video bora.
Video ya nyimbo hiyo inatarajia kutoka rasmi April 5 siku ya pasaka.
https://www.youtube.com/watch?v=Z0N190dGOjU
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza>>>twitter Insta Facebook