Mwimbaji Diamond Platnumz Jumanne ya January 21 2014 alitimiza ahadi yake kwa watoto walioshinda kwenye tamasha la watoto la Xmas aliloliandaa na kukutana na watoto kwenye stage ambayo pia alishindanisha wanaojua kucheza na kuimba wimbo wake wa ‘number one’ a.k.a ngololo kwenye viwanja vya Leaders Club Dar es salaam.
Walipatikana washindi ambao ilikua ni ahadi yake kuwalipia ada na kuwasomesha kwenye shule nzuri za kisasa zenye kiwango kizuri cha elimu na kweli amefanya hivyo kwa kuwapeleka mwenyewe shuleni na kuwalipia ada ambayo inazidi milioni sita na laki saba kwa Wanafunzi wote wawili.
Ahadi yake ni kuwasomesha mpaka darasa la saba peke yake.
Hizi ni baadhi ya picha zinazomuonyesha Diamond akiwakabidhi watoto hao kwa Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Mercy Githirua na picha ya pamoja na wanafunzi wa East Africa International School.
Mwalimu mkuu msaidizi ameiambia millardayo.com kwamba ilibidi wapige kengele na Wanafunzi kukusanyika mstarini kwa ajili ya kumsikia Diamond kwa dakika kadhaa.
Mwalimu huyu msaidizi aitwae Nelson anasema ‘mmoja wa Wanafunzi hawa yuko darasa la nne na mwingine darasa la tano, Diamond alipopata nafasi ya kuongea na Wanafunzi baada ya kuitwa maalum kumsikiliza, aliwapa moyo na kuwapa ushauri kuhusu dunia ya sasa, Wazazi wa wale watoto pamoja na uongozi walikubaliana watoto waanze shule Ijumaa kila kitu kikiwa kimekamilika’