Ni stori iliyochukua headlines kwenye upande wa soka September 27 katika mechi kati ya Azam FC dhidi ya Mbeya City mchezo uliochezwa katika uwanja wa Azam Complex Mbande Chamazi, nahodha wa Mbeya City Juma Nyoso alimfanyia kitendo cha kidhalilishaji nahodha wa Azam FC John Bocco, licha ya kuwa muamuzi hakuona ila kupitia picha za mnato na kanda za video tukio hilo lilinaswa na kusambaa katika mitandao ya kijamii.
Sasa leo Sept 29 msanii wa Bongo Fleva Diamond Platnumz akiongea na ripota wa millarayo.com amezungumza kuchukizwa kwa kitendo hicho cha udhalilishaji na kusema….‘Mimi sio mfuatiliaji sana wa mpira Tanzania sio tu Tanzania bali ulimwengu mzima kwasababya kazi zangu za muziki kuniweka katika hali ya kuwa busy sana ila naangalia mara moja moja tu kama mechi kubwa za fainali na nyingine’ – Diamond Platnumz
‘Nimekutana na picha kuna mtu alinitumia sasa nikaanza kujiuliza kwani hii ilikuaje ndipo kuna mtu akaanza kunifafanulia kwamba hivi na hivi, unajua nimejisikia vibaya sana tutaweza vipi kukuza sanaa yetu tutaweza vipi kukuza michezo kweli baada ya kucheza mpira tunaanza kufanya vitu kama hivyo vya udhalilishaji tunatakiwa tucheze mpira na tuwe mifano bora kila siku wenzetu wanatucheka kiukweli nimejisikia vibaya na si kitendo kizuri kwa mwanaume mwanzao kumfanyia mwenzako nyuma ya Maumbile’ – Diamond Platnumz
Unaweza uka bonyeza play kumsikiliza Diamond Platnumz
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE