Habari za Mastaa

Hatua nyingine kwa Diamond Plutnumz.

on

diamondplaDiamond Plutnumz bado ameendelea kudhihirishia ulimwengu kwamba anapiga hatua kulingana na juhudi alizonazo kwenye muziki,hili ni shavu lingine,kwa sasa Diamond ameteuliwa kuwa moja kati ya wasanii wanaootoka Afrika na watakaoshiriki katika Tuzo za muziki zitakazofanyika huko Eisemann Center Dallas Nchini Marekani

Tuzo hizi zinatarajiwa kufanyika July 26 2014 na pia inategemewa kuwakutanisha wasanii mbalimbali kutoka Africa Magharibi Kusini na sehemu zingine na taarifa iliyopo ni kwamba Mc wa shughuli hiyo atakuwa ni mchekeshaji kutoka Nigeria Basket Mouth pamoja na Na Mrembo Pia Muigizaji Kutoka Nollywood Juliet Ibrahim.

diiiiShow hiyo inategemewa kuanza saa 2 kamili usiku na hii ni miongoni mwa show kubwa kwa wa Africa maana Itakusanya wadau kibao wa muziki wa kiafrika Duniani kutakua na Wanamuziki,Ma producer,Ma Manager,Dj’s Na kila anaeendeleza Tamaduni za Kiafrica.

Unaambiwa pia Wageni kutoka Mataifa 17 ya Africa wanatarajia kutoka Miji ya mbali mbali ya Nchini Marekani kuhudhuria Tuzo Hizo Ambapo kwa hapa Tanzania tunatarajia kuwakilishwa na Diamond Platinum.

Diamond pia wiki chache zilizopopita alitoa Sample ya ClothingLine yake yenye nembo ya Wasafi Classic Baby.

diamonnn

Hizi ni sekunde kadhaa Diamond akielezea mchakato huo wa tuzo hizo.

Tupia Comments