Waziri wa Maliasili na Utalii Dr Hamis Kigwangalla amehoji kuhusiana na taarifa ya MO Dewji wa Simba SC kudai kuwa analipa mishahara ya karibia bilioni 4 kwa mwaka, taarifa hiyo ilitoka MO Dewji alipotangaza kujiuzulu jana kabla ya leo kufuta uamuzi huo, hivyo Kigwangalla ambaye ni shabiki wa Simba SC alihoji hizo bilioni 4 kama ni zile sehemu ya pesa za uwekezaji wa Bilioni 20 MO?
“Poleni wanasimba wenzangu, ‘kisukari kimetuvuruga’, hivi kuna mtu anaweza kunisaidia? Hii mishahara ya 4bn iliyolipwa na Mo inalipwa kwa makubaliano gani? Isijekuwa ndiyo katika ile 20bn ya manunuzi ya hisa 50%, ama manunuzi yalikwishafanyika? Anavyojitoa, italipwaje? #NguvuMoja”
MO Dewji inadaiwa kuwa alifanya maamuzi hayo kutokana na kile kinachodaiwa na wengi timu hiyo kupoteza mchezo wa fainali ya Mapinduzi Cup 2020 dhidi ya Mtibwa Sugar kwa kufungwa goli 1-0, kutofanya vizuri katika mchezo wa January 4 2020 dhidi ya Yanga SC kwa kutoka sare ya 2-2 lakini kubwa ni kuishia round ya awali ya michuano ya CAF Champions League na kutolewa na UD Songo ya Msumbiji.
USHAURI WA RIDHIWANI KIKWETE KWA MO DEWJI BAADA YA KUJIUZULU