Wataalamu nchini Uingereza wameeleza kuwa kazi za nyumbani zinaweza kuwa msaada mkubwa sana katika kupunguza uzito wa mwili ambao kimsingi husababisha matatizo mbalimbali ya afya ukilinganisha na kufanya mazoezi gym, kukimbia, kuruka kamba na mengineyo.
Utafiti mpya umeeleza kuwa mtu anaweza kukata mafuta yaani ‘calories’ 600 ndani ya mwili kwa kufanya kazi nyingi na za kutumia nguvu kwa masaa mawili tu mfululizo kiwango ambacho ni mara mbili ya mtu anayekimbia kilometa 5 ambaye kwa kawaida huwa ana uwezo wa kukata calories 374.
Utafiti huu ambao umefanywa na taasisi ya kutunza nyumba kwa ubora ‘Good Housekeeping Institute (GHI)’ nchini humo pia umeeleza kuwa kufanya usafi kwenye madirisha, kudeki pamoja na kusafisha choo na bafu huongoza katika kuchoma mafuta hayo.
Ulipitwa? MBUNGE MSUKUMA: Kuhusu kuishia Darasa la Saba, kaeleza kila kitu
Hii je? BREAKING: Maagizo ya Waziri Nchemba baada ya Lissu kupigwa risasi