Habari za Mastaa

Mixtape ya Drake na Future imegusa nafasi ya juu kwenye chati ya Billboard Marekani!

on

Mwaka huu umekuwa poa sana kwa mastaa wa muziki wa Hip Hop Marekani Drake na Future… mixtape yao ya What a Time to Be Alive imeweka headlines nyingi sana Marekani na kwenye chati mbalimbali za muziki moja wapo ikiwa chati ya Billboard.

June 20, 2015 -- ATLANTA -- Drake makes a surprise appearance Future at Birthday Bash 20. (Akili-Casundria Ramsess/Special to the AJC)

What a Time to Be Alive mixtape ya Future na Drake imegusa no.1 kwenye countdown chart ya Billboard 200! Mixtape hiyo ambayo awali iliuza zaidi ya copy 375,000  chini ya mategemeo ya wasanii hao imefanikiwa kugonga namba moja kwenye chati hiyo ndani ya wiki chache.

drizzfewtch3

Drake.

Kwa Drake na Future mwaka huu umekuwa poa sana kwao kwani miezi michache iliyopita mixtape ya Drake ‘If You Are Reading This Its Too Late’ iligusa no.1 kwenye chati hiyo ya Billboard 200Future naye hakuwa mbali sana kwani hata mixtape yake ya DS2 LP ilifanikiwa kuhit nafasi ya kwanza pia kwenye chati hiyo!

drizzfewtch4

Future.

Kwa mujibu wa mtandao wa Billboard Future na Drake ni wasanii pekee mwaka huu wenye no.1 mbili kwenye chat ya Billboard 200 na mara ya mwisho msanii wa hip hop kushika nafasi hiyo mara 2 ndani ya mwaka mmoja alikuwa ni rapper Jay Z mwaka 2004!

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasamuziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata, pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>> YouTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments