Kamati ya uchaguzi ya shirikisho la soka Ivory Coast (FIF) imemuengua mchezaji wa zamani wa Chelsea na timu ya taifa ya Ivory Coast Didier Drogba katika kinyang’anyiro cha kuwania Urais wa FIF kwa sababu ya kudaiwa document zake hazikukidhi vigezo.
Drogba inadaiwa ndio anapewa kipaumbele zaidi katika mbio za kuwania Urais wa FIF katika uchaguzi mkuu wa FIF unaotarajia kufanyika September 5 2020.
Kwa kuenguliwa huko basi Drogba abapoteza nafasi ya kuwania nafasi ya Urais na kumuacha Sory Diabate na Idriss Diallo katika mbio za kuwani urais huo.