Mshambuliaji wa kimataifa wa Ivory Coast Didier Drogba ambaye pia amewahi kuitumikia klabu ya Chelsea ya Uingereza kwa miaka kadhaa sasa ameamua kuendeleza maisha yake ya soka Canada na ataanza kuonekana katika Ligi Kuu ya Marekani MLS.
Taarifa zimethibitisha kuwa Drogba amekubaliana na klabu Montreal Impact na atajiunga na timu hiyo kwa mkataba wa miezi 18, Drogba amekuwa akiwindwa na timu zinazoshiriki Ligi Kuu Marekani toka mwaka 2012 na alikataa mshahara wa dola milioni 7.5 kwa mwaka na kutimkia China.
Rais wa klabu ya Montreal Impact Joey Saputo amethibitisha Drogba kujiunga na kikosi chao.
“Ni heshima kumkaribisha Drogba katika klabu ya Montreal Impact, toka mazungumzo yetu ya kwanza nazungumza nae, nilijisikia kwamba kiukweli alitaka kuichezea Montreal”>>>Joey Saputo
Drogba anaungana na mastaa wengine wa soka waliowahi kutamba katika Ligi Kuu Uingereza, mastaa hao ni Frank Lampard na Steven Gerrard bila kumsahau mkali mwingine kutokea Italia Andrea Pirlo amabo pia wametimkia Marekani.
Nitakutumia stori zote ukibonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.