Tunayo stori kutokea Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) John Maruru ameieleza mahakama hiyo kuwa watu wanne waliodaiwa na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe kuwa waliuliwa na askari polisi huko mkoani Kigoma, wapo hai na watakuja kutoa ushahidi.
SSP Maruru ambaye ni mpelelezi wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, ameyaeleza hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi wakati akitoa ushahidi katika kesi ya uchochezi inayomkabili Zitto Kabwe.
Katika ushahidi wake akiongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Nassoro Katuga, Maruru amedai watu hao wanne ambao Zitto alidai kuwa walikuwa majeruhi na kupelekwa kituo cha afya Nguruka, na kwamba polisi waliwachukua na kuwaua sio kweli. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Aprili 25, 2019 kwa ajili ya kuendelea na ushahidi.