Top Stories

“Zoezi la vitambulisho vya taifa lisihusishwe na siasa” – Mwigulu Nchemba

on

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dr. Mwigulu Nchemba amewataka Watanzania kujiandikisha kupata kitambulisho cha Taifa kwani si zoezi la hiari bali la lazima kwa Mtanzania aliyeko ndani ya mipaka ya nchi ili kutambuliwa.

Waziri Mwigulu amewataka wananchi kuacha mazoea ya kutafuta kutambuliwa pindi wanapokuwa na shida hasa za kutaka hati ya kusafiria au migogoro ya ardhi pale anapoambiwa yeye si raia wa Tanzania .

“Zoezi hili la kujiandikisha na kupata kitambulisho ni bure, pasitokee kiongozi yeyote wa wilaya na vijiji kuchangisha fedha wananchi ili wapate fomu za kujiandikisha na wala zoezi hili lisihusishwe na siasa.” – Dr.Mwigulu

“Huu ni uhujumu uchumi, Wote tutawachukulia hatua” –Naibu Waiziri Mwanjelwa

 

Soma na hizi

Tupia Comments