Habari za Mastaa

Baada ya video za Jux na Snura, hii ndiyo video nyingine ya Bongo iliyofungiwa.

on

Screen Shot 2014-02-20 at 11.06.26 AMMwanzoni mwa mwaka 2014 kumeripotiwa video kadhaa za Tanzania kufungiwa huku sababu kubwa ikiwa haijatajwa moja kwa moja,miongoni mwa watu waliofungiwa video zao ni pamoja na Jux ‘Uzuri wako’ na video ya Snura ‘Nimevurugwa’.

Millardayo.com iliwahi kwenda Basata kujua taratibu zinazopelekea kufungiwa kwa video hizo ili kujua pia vigezo vinavyotumika kufungia video hizo,Basata walisema wao hawahusiki na ufungiaji wa video na kusema kazi hyo inafanywa na Bodi ya Filamu Tanzania.

February 19 Kupitia 255 ya Clouds Fm Dully sykes ambaye ni miongoni mwa wasanii wakongwe wa muziki wa Bongo Fleva ali-amplify kuhusu kufungiwa video yake ya Kabinti Special ambapo alisema>>’video yangu imefungiwa wanasema kwa ajili ya maadili,wanasema sijui Diamond amevaa fulana sijui wameandika nini na video Q2ueen sijui amevaa swimming costume nguo ambazo hazipo kimaadili’

‘Unajua sisi Watanzania tukifanya hivi kila siku tutakuwa hatuna maendeleo kwa sababu ukiangalia South Africa uchumi wao unapanda kwa ajili ya muziki,pia unachangia muziki kupanda’

‘Nigeria pia unachangia muziki kupanda,muziki umepanda na uchumi umepanda pia hata Kenya hapo,hata Uganda kwa ajili wao wanamuziki wanafanya uchumi upande na nchi yao inapendeza kuona kwamba mastaa wazuri ambao wanafanya kazi nzuri kupigwa katika nchi zote Duniani kujulikana’

‘Unajua msanii anapojulikana anapojulikana ametoka nchi fulani,mtu mwingine Tanzani haijui akimuona Tunda katika MTV anajua kuna nchi inaitwa Tanzania,kwa hiyo sisi Watanzania na serikali inabidi tuendelee mbele kama wai wanavyoweza tunataka watuachie tuangalie maendeleo ya sisi wanamuziki tunafika wapi’

‘Tunabidi na sisisiku moja moja tuwe na sehemu zetu kubwa,sasa wakitaka basi mtu akivaa swimming costume hayupo mtupu anataka video isipigwe,hii si mara ya kwanza kwa sababu hata Nyambizi waliifungia kwa kweli mimi walivyonikatisha tamaa ile sikutaka tena kuendelea nikasema ngoja niangalie kitu kingine cha kufanya’

‘Kwa sababu kama nchi yangu inanikatisha tamaa nchi gani itakuja kunisupport?kiukweli kabisa mimi naongea kama kiongozi wa wana bongo flava Tanzania muziki wa kuimba’

‘Serikali inabidi ituangalie sisi tunaofanya muziki ili kuipandisha nchi yetu ili iwe kwenyue nafasi nzuri kiukweli kabisa wananchi watuache ili tufanye kazi ili kuisaidia nchi yetu kufika mbali,sasa wanawake wakiwa wanavaa madila kwenye nyimbo za kisasa itakuwaje’.

Itazame hapa video yenyewe on AyoTV.

Tupia Comments