Duniani

Top 10 ya viwanja vya ndege bora zaidi duniani kwa mwaka 2017

on

March 14, 2017 zilitangazwa tuzo ambazo hutolewa kwa Airport bora zaidi kwa mwaka ambapo Changi Airport imeshinda tuzo hiyo kwa mara ya tano mfululizo kuwa “World’s Best Airport” katika tuzo  za Skytrax World Airport Awards 2017.

Tuzo zimetengazwa mjini Amsterdam March 14 baada ya utafiti ulioegemea kwa mamilioni ya wasafiri duniani kote.

Nimekuwekea hapa list kamili ya Skytrax World’s Best Airport Award 2017.

1: Singapore Changi Airport – Singapore

Changi Airport umeshinda tuzo ya Skytrax World’s Best Airport kwa mara ya tano mfululizo ambapo miongoni mwa mambo yanayowavutia wasafiri ni uwepo wa ukumbi wa cinema ambao huonesha movie mpya kila siku bure, swimming pool na bustani nzuri ya vipepeo.

2: Tokyo International Airport Haneda – Japan

Haneda Airport inakamata nafasi ya pili ikiwa ni moja kati ya airport mbili kutoka Japan kwenye list hii.

3: Incheon International Airport – Seoul, Korea Kusini

Incheon International Airport imekuwa katika tatu bora tangu 2013.

4: Munich Airport – Ujerumani

Munich Airport imeanguka nafasi moja mwaka huu na kuifanya kuwa namba 4.

5: Hong Kong International Airport

Uliwahi kushinda namba moja miaka ya nyuma lakini mwaka huu Hong Kong International Airport imeshika nafasi ya tano ikitetea nafasi hiyo iliyowahi kuikamata 2016.

6: Hamad International Airport – Doha, Qatar

Ulifunguliwa rasmi 2014 na sasa Hamad International Airport iliyopo Doha imevuka nafasi nne na kukamata nafasi ya sita – mwaka 2015 ulikuwa katika nafasi ya 22.

7: Chubu Centrair International Airport – Nagoya, Japan

Chubu Centrair International Airport upo umbali wa mile 22 kusini ya Nagoya katikati ya Japan na unakamata nafasi ya 7, kwa mujibu wa SkyTrax.

8: Zurich Airport – Switzerland

Katika list ya 2017 Zurich Airport imeanguka nafasi moja baada ya 2016 kukamata nafasi ya 7.

9: London Heathrow Airport – Uingereza

London Heathrow Airport ndiyo airport iliyokuwa busy zaidi Ulaya kwa kusafirisha abiria wengi na katika Skytrax World Airport 2017 inakamata nafasi ya 9.

10: Frankfurt Airport – Ujerumani

Miongoni mwa airport zilizokuwa busy Ulaya Frankfurt Airport ipo na inakamata nafasi ya 10 kwenye Skytrax World Airport Awards 2017.

Video: Ulikosa kuiona Treni ya kifahari ilivyoondoka DSM kuelekea Afrika Kusini? Nimekuwekea hapa chini bonyeza play kuitazama.

BREAKING NEWS zote na stori za mastaa utazipata kwa Reporter wako MillardAyo, hakikisha umejiunga na mimi kwenye Facebook, Twitter, Instagram, Snapchat, Youtube, APP kwenye ANDROID na IOS kote huko kwa jina hilohilo la @millardayo

Soma na hizi

Tupia Comments