July 27 2015 Mbunge James Mbatia ambaye ni mmoja ya Viongozi wa juu wa Jumuiya ya Vyama vinavyounda umoja wa UKAWA aliongea maneno haya baada ya Viongozi wote kukaa Kikao na kukubaliana >>>> “Nachukua fursa hii kumualika Mheshimiwa Lowassa ajiunge na UKAWA na tuko tayari kushirikiana nae kuiondoa CCM madarakani”— James Mbatia.
Viongozi wa UKAWA wamekutana Bahari Beach Dar July 28 2015, wakiwa wameongozana na Mbunge wa Monduli, Edward Ngoyai Lowassa na kuumaliza utata wa maswali mengi kuhusu uamuzi wa Lowassa baada ya jina lake kutopitishwa kwenye Urais CCM.
Mbunge Edward Lowassa alitumia muda mfupi tu kuthibitisha kujiunga CHADEMA, na hii ni sehemu ya alichokisema.
Nimetumia wiki mbili kutafakari hatma yangu ktk Siasa, najua wengi wamesubiri kwa hamu. #TZALiveUpdates #LowassaCDM
— millard ayo (@millardayo) July 28, 2015
Watu wangu wamesema fanya maamuzi magumu.. Namshukuru Mke wangu na familia wamekuwa na mimi ktk kipindi kigumu- #TZALiveUpdates #LowassaCDM — millard ayo (@millardayo) July 28, 2015
Nawashukuru watu wengi waliojitokeza kuniunga mkono wakati natafuta wadhamini- #TZALiveUpdates #LowassaCDM
— millard ayo (@millardayo) July 28, 2015
Uchaguzi wa Mgombea CCM ulijaa chuki dhidi yangu, Kamati ya Maadili haikutakiwa kuchagua Mgombea- #TZALiveUpdates #LowassaCDM — millard ayo (@millardayo) July 28, 2015
Kilichotokea Dodoma kinaitwa ‘kubaka Demokrasia’ – #TZALiveUpdates #LowassaCDM
— millard ayo (@millardayo) July 28, 2015
CCM iliwatumia vijana wachache kunikashifu na baadae wakapewa Madaraka makubwa- #TZALiveUpdates #LowassaCDM — millard ayo (@millardayo) July 28, 2015
Kibaya zaidi kilikuwa kuwanyima Wagombea 38 wa CCM haki ya kujieleza mbele ya Kamati Kuu- #TZALiveUpdates #LowassaCDM
— millard ayo (@millardayo) July 28, 2015
Nilinyimwa haki ya Msingi ya kusikilizwa na kujieleza CCM, nitakuwa mnafki kusema nina imani na CCM –#TZALiveUpdates #LowassaCDM — millard ayo (@millardayo) July 28, 2015
CCM niliyoiona Dodoma sio CCM iliyonilea Kisiasa, mimi km Mtanzania mwenye Uhuru nasema sasa basi- #TZALiveUpdates #LowassaCDM
— millard ayo (@millardayo) July 28, 2015
Mwalimu NYERERE alisema CCM sio baba yangu wala mama yangu,nimeamua kuanzia leo naondoka CCM na kujiunga CHADEMA-#TZALiveUpdates #LowassaCDM
— millard ayo (@millardayo) July 28, 2015
Namshukuru sana James MBATIA na Viongozi wa UKAWA kwa kuniamini na kunipokea- #TZALiveUpdates #LowassaCDM — millard ayo (@millardayo) July 28, 2015
Naamini UKAWA tutaondoa mfumo wa Utawala wa Chama kimoja, naomba Watz wajiunge nasi ktk SAFARI YA MATUMAINI- #TZALiveUpdates #LowassaCDM
— millard ayo (@millardayo) July 28, 2015
Kulipa kisasi ni upuuzi, umefanya nini mpaka useme nitalipa kisasi? Waulizeni wamefanya nini nilipe kisasi?- #TZALiveUpdates #LowassaCDM
— millard ayo (@millardayo) July 28, 2015
Msiwatishe, kama wamefanya madhambi yao waambieni nimewasamehe mimi sitalipa kisasi- #TZALiveUpdates #LowassaCDM
— millard ayo (@millardayo) July 28, 2015
Nitakutumia stori zote ukibonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.