Michezo

Baba mzazi wa Emiliano Sala amefariki miezi mitatu baada ya kifo cha Sala

on

January 22 2019 mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina aliyekuwa anaichezea club ya Nantes ya Ufaransa Emiliano Sala, aliripotiwa kupoteza maisha kufuatia kupotea kwa ndege yao binafsi waliyokuwa wanasafiria kutoka Nantes kwenda Wales kuanza kuitumikia timu ya mpya ya Cardiff City akiwa na rubani wake.

Taarifa za kifo cha Emiliano Sala zilipokelewa kwa masikitiko makubwa sana na kila mwanafamilia wa michezo hususani wachezaji soka, leo April 26 2019 zimeripotiwa taarifa mpya kuwa baba mzazi wa mchezaji huyo Horacio amefariki dunia kwa tatizo la moyo ikiwa ni miezi mitatu imepita toka kitokee kifo cha mtoto wake Emiliano Sala.

Horacio Sala mwenye umri wa miaka 58 amefariki akiwa nyumbani kwake Progreso Argentina, baba mzazi wa mchezaji huyo Horacio amefariki usiku wa Jumanne ya April kwa shambulio la moyo, indaiwa kuwa shambulio hilo la moyo lililopelekea kifo cha mzee Horacio ambaye alikuwa dereva wa malori zamani kinatokana na msongo wa mawazo kutokana na kifo cha kusikitisha cha Emiliano Sala.

Emiliano Sala alijiunga na Cardiff City ya Wales January kwa dau la pound milioni 15 akitokea Nantes FC ya Ufaransa na baada ya hapo kurejea Nantes kwa ajili ya kuwaaga wachezaji wenzake na January 21 ndipo akaanza safari ya kurejea Cardiff kuanza maisha mapya ndio ndege yao Piper Maliba akiwa na rubani wake David Ibbotson ikapotea kwenye rada wakiwa pwani ya Guenmay.

Simba na Yanga za kataa kuungana ili kucheza na Mabingwa mara 5 wa Europa League May 23

Soma na hizi

Tupia Comments