Shakira amekuwa mtu wa kwanza duniani kwenye mtandao wa Facebook kupata Likes milioni 100 katika ukurasa wake.
Nyota huyo wa muziki kutoka nchini Columbia amevunja rekodi hiyo siku nne tu baada ya kufanya onyesho katika fainali za michuano ya kombe la dunia nchini Brazil.
Shakira aliyemzidi Rihanna kama Star wa kwanza Facebook mwezi Machi mwaka huu akiwa na watu milioni 86.8 amesema kuwa anajisikia fahari kubwa kufikia rekodi hiyo kwasababu hiyo ni sehemu pekee inayomuunganisha na mashabiki wake kutoka sehemu mbalimbali duniani.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta FB