Baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kutangaza rasmi zuio la matumizi ya mifuko ya Plastiki nchini, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais ( Muungano na Mazingira), January Makamba amesema katazo hilo limepokelewa vizuri na wadau na lilisubiriwa kwa hamu.
Waziri Majaliwa amesema itakuwa ni marufuku kutengeneza, kuingiza, kuuza na kutumia mifuko ya plastiki kwa ajili ya kubebea bidhaa za aina yoyote na matumizi yake yatakoma ifikapo Mei 31, 2019.
Akizungumza na waandishi wa habari, Waziri Makamba amesema wamekutana na wadau wa uzalishaji wa mifuko ya plastiki na wamelipokea katazo hilo vizuri kwani hatua hiyo imechukuliwa hasa kwa ajili ya kulinda afya.
“Mtu ambaye amezalisha na katazo limekuja hatuna namna ya kumsaidia, kwani unapo Bet kwamba serikali haitasimamia kauli yake basi kama ume Bet umepoteza na hakuna kingine cha kusema,“amesema.