Mix

Video: RC Makonda kafunguka kuhusu hizi bilioni 90 kwenye wilaya ya Kigambo

on

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amemshukuru Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutoa Kiasi cha Shilingi Bilioni 90 za ujenzi wa Barabara kwa kiwango cha Lami kuanzia Kibada kuzunguka Mwasonga na Kisarawe Two ikiwa nisehemu ya kutatua kero za ubovu wa barabara kwa wananchi wa Wilaya hiyo.

RC Makonda ameeleza hayo leo wakati wa Ziara ya Ukaguzi wa Miradi ya maendeleo Wilaya ya Kigamboni na kueleza kuwa Serikali imedhamiria kufanya mji wa Kigamboni kuwa wa kisasa hivyo amewahimiza wananchi kuhakikisha wanaepuka ujenzi holela, uuzaji wa viwanja bila taratibu pamoja na Ujenzi bila Vibali.

 

Soma na hizi

Tupia Comments