
Kwani Floyd Mayweather kafilisika? kaamua kuususa mkanda wake? au ndio mwendelezo wa zile mbwembwe zake? Kweli kaamua kuuachia mkanda wake hivihivi kisa deni la Mil 446?

Story ya mwishomwisho kusikika kuhusu yeye ilihusu Shirikisho la Ngumi Duniani WBO kutangaza kumvua mkanda alioshinda baada ya kumpiga Manny Pacquiao kutokana na deni la Dola 200,000 (ni kama Tshs. 446) ambazo ilitakiwa alipie kama kodi baada ya pambano lake na Manny Pacquiao!!
Tukiachana na stori hizo najua kuna mastory mengi kuhusu jamaa kustaafu, maswali kuhusu nani atapanda nae jukwaani hivi karibuni.. ninayo hii list ya Mabondia ambao wametajwa kwamba huenda mmoja wao akapanda kuzipiga nae kabla hajastaafu.
Kiukweli kwenye hii list hakuna mwenye rekodi mbaya, kila mmoja ni mkali yani.






Wakati utafika na tutajua tu nani atakutana ulingoni na mbabe huyu wa karne, swali ni kwamba atakubali rekodi yake ya ushindi wa mapambano 48 iharibike?
Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.