Premier Bet
TMDA Ad

Michezo

Kutokea Algeria, Morocco na Hispania Ulimwengu, Msuva na Chilunda kuhusu Kundi C AFCON 2019

on

Baada ya kumalizika kupangwa kwa droo ya makundi ya fainali za mataifa ya Afrika 2019 (AFCON 2019) zitakazofanyika nchini Misri June 21 hadi July 19, huku Tanzania ikiangukia Kundi C lenye timu za Senegal, Algeria na Kenya, AyoTV imefanikiwa kuwapata baadhi ya wachezaji wa Taifa Stars wanaocheza nje ya Tanzania na kuwauliza mtazamo wao Kuhusu Kundi C.

AyoTV imeongea na mshambuliaji wa Taifa Stars Thomas Ulimwengu anayecheza soka la kulipwa nchini Algeria katika club ya JS Saoura, Simon Msuva anayeichezea Taifa Stars na club ya Difaa El Jadid ya Morocco sambamba na Shaban Iddi Chilunda mchezaji wa CD Tenerife ya nchini Hispania lakini kwa sasa yupo kwa mkopo CD Izzara.

Rais Karia kaiomba kamati ya RC Paul Makonda kuhamishia nguvu kwa Serengeti Boys

Soma na hizi

Tupia Comments