Top Stories

Rais wa zamani wa Korea Kusini amehukumiwa miaka 24 jela

on

Rais wa zamani wa Korea Kusini  Park Geun-hye, amehukumiwa miaka 24 jela baada ya kukutwa na hatia katika matumizi mabaya ya madaraka na kusababisha nchi kushuka kiuchumi.

Park Geun-hye aliondolewa madarakani mwaka jana baada ya kutuhumiwa kutumia vibaya wadhifa wake na kusababisha kuanguka kwa uchumi.

 

Rafiki yake Choi Soon-sil, anayehusishwa na kashfa hiyo, alihukumiwa wiki mbili zilizopita hadi miaka 20 jela kwa kupokea hongo iliyotolewa na makampuni ya Korea Kusini, ikiwa ni pamoja na makampuni yai Samsung na Lotte.

Katika mashtaka yake, mwendesha mashtaka alimshtaki rais wa zamani kuwa “alisababisha mgogoro wa kitaifa kwa kuacha mtu ambaye hajawahi kushiriki katika usimamizi wa umma kuongoza nchi”.

Kesi ya rais wa zamani Korea Kusini ilifunguliwa mwezi Mei mwaka jana. Mahakam inatarajia kutoa uamuzi wake kabla ya mwezi April mwaka huu.

Shughuli atazofanya Rais Magufuli Arusha akiwa na Jeshi la Polisi

Soma na hizi

Tupia Comments