Top Stories

Jacob Zuma amefikishwa Mahakamani

on

Aliyekuwa rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amefikishwa mahakamani leo katika mji wa Durban ili kujibu mashtaka ya rushwa, udanganyifu na kujitajirisha kinyume cha sheria. Kesi hii inasikilizwa kwa mara ya kwanza na inahusu biashara ya zamani ya mauzo ya silaha tangu miaka ya 1990.

 Rais wa zamani wa Afrika Kusini anashutumiwa kupokea rushwa kutoka kwa Thomson CSF – jina la zamani la kampuni ya Thales – katika mpango wa mkataba wa mauzo ya silaha wenye thamani ya karibu Euro Bilioni 4 ulioafikiwa mnamo mwaka 1999.

Wakati huo, Jacob Zuma alikua makamu wa rais wa nchi ya Afrika Kusini. Anashutumiwa kuwa alipokea jumla ya euro milioni 50 kutoka kampuni ya Ufaransa ya Thales. Kwa upande mwingine, aliahidi kupatishia zabuni kampuni hiyo ya Thales.

Kwa jumla, Afrika Kusini iliamua kutumia zaidi ya dola bilioni 10 kurejelea upya silaha zake. Silaha ambazo nchi hiyo haikuweza kuzihitaji wakati huo na ambazo hazitumiwi leo. Lakini sababu kuu ni kwamba zaidi ya dola milioni 300 (hongo) zililipwa wakati wa mikataba hii.

Mambo 3 Kesi ya Rais Simba, Mashtaka yamebadilishwa, anatembea kwa kushikiliwa

Soma na hizi

Tupia Comments