Club ya Arsenal Jumapili ya April 7 2019 ilicheza game yake ya 32 ya Ligi Kuu England msimu wa 2018/2019 ugenini dhidi ya Everton lakini pamoja na kuwa Arsenal ina mastaa na ilipewa nafasi kubwa na wachambuzi wa soka kushinda mchezo huo wamejikuta wakipoteza 1-0 lililofungwa na Jagielka dakika ya 10.
Kipigo hicho hakijawashitua sana watu pamoja na matarajio yao kuwa makubwa kwa Arsenal zaidi ya Everton, kwani kupoteza ni hali ya kawaida katika mchezo, kinachowashangaza wengi ni rekodi aliyonayo Arsenal kwa sasa anapocheza game za ugenini kwani ana wastani mdogo sana wa kushinda kuliko kupoteza.
Arsenal msimu wa 2018/2019 wa Ligi Kuu England katika mechi tisa za ugenini zilizopita, ameshinda mchezo mmoja pekee, sare tatu na amepoza mara tano, hii ni rekodi mbaya kwa kocha Unai Emery hususani kipindi hiki anachowania kusalia TOP 4 mwisho wa msimu ili apate tiketi ya kucheza UEFA Champions League.
“Nina uhakika tunaweza kushinda Lubumbashi na kufuzu”- Kocha Simba SC